Meneja Masoko wa maduka ya Woolworths Tanzania,Edwina Barongo akisisitiza jambo kwa wateja waliofika katika Uzinduzi wa punguzo la bei ya bidhaa zote zinazouzwa katika Maduka yote ya Woolworths yaliyopo Arusha na Dar es Salaam, Punguzo hilo litadumu kwa muda wa wiki Nne ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mgeni rasmi (Loyal Customer) Manfred Ngantunga (kulia) akizindua duka la Woolworths lililopo mtaa wa Ohio jengo la PPF Tower ikiwa ni sehemu ya kuzindua punguzo la bei nafuu kwa bidhaa zinazouzwa na kampuni hiyo katika maduka yaliyopo Arusha na Dar es Salaa.Katikati ni Meneja Mkuu wa Woolworths Tanzania Joehans Bushiri na Mkurugenzi wa fedha Samson Katemi(kushoto).Uzinduzi huo wa Punguzo la bei kwa asilimia 50 utadumu kwa muda wa wiki Nne ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mteja wa muda mrefu wa bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Manfred Ngantunga (katikati) akikabidhiwa zawadi na mfanyakazi wa duka hilo, baada ya kuzindua punguzo la bei la bidhaa kwa asilimia 50%zinazouzwa kwenye maduka ya hayo Tanzania, Kulia ni Meneja Mkuu wa Woolworths Joehans Bushiri,Hafla ya uzinduzi ilifanyika makao makuu ya woolworths jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Woolworths Tanzania, Joehans Bushiri akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa punguzo la bei kwa bidhaa zinazouzwa katika maduka yote ya Woolworth, kwa kipindi cha wiki Nne ikiwa ni sehemu ya ponguzo la kununua bidhaa bora kwa kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka.Hafla ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwakweli wamefanya jambo zuri, ukizingatia nguo zao zina ubora wa hali ya juu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...