Na Maneno Selanyika, Dar es Salaam

SERIKALI na wadau wa sekta ya elimu wanatakiwa kuboresha shule kongwe zilizopo hapa nchini kwa kuwa zina mchango mkubwa katika kulifikisha Taifa hapa lilipo.

Wasomi wengi waliostaafu, wanasiasa, wabunge na viongozi waliopo sasa madarakani wengi wao walisoma kwenye shule hizo ambazo kwa sasa zinakabiliwa na changamoto nyingi hasa za kitaaluma, hivyo kupoteza umaarufu wake.

Ikumbukwe tu kwamba shule ni sehemu ya kumwandaa kijana ili baadae aweze kukabiliana na changamoto za mazingira yanayomzunguka.

Ukizitaja shule hizo za zamani ni lazima Azania Sekondari iwepo kwani ni shule ambayo May 2 mwaka huu itatimiza miaka 81  tangu ianzishwe mwaka 1943.
Nyingine ni Tambaza, Jangwani na Zanaki.

Historia ya Azania

Akizungumza na MTANZANIA kuhusu maadhimisho ya miaka 81 ya Shule ya Sekondari Azania, Mkuu wa Shule, Benardi Ngozye anasema shule hiyo ilianzishwa na watu ambao walikuwa ni jamii ya Wahindi Weusi waliotokea nchini India, ambapo wakati huo ilikuwa ikiitwa Government India Primary School – Mtendeni. 

Mwaka 1939 shule hiyo ilibaddilishwa ikaitwa Government India Secondary School, ambapo baada ya mji kukua ikagawanywa mara mbili ya wasichana ambayo ni Jangwani kwa sasa na wavulana – Azania.

Ngozye anasema mwaka 1952 wavulana walihamishwa kutoka Mtendeni wakajengewa shule yao ambapo iliandikisha wanafunzi sita tu wa Kiafrika ndipo jina la Azania likazaliwa.

Anasema shule hiyo wakati ikianzishwa asilimia 95 ya walimu walikuwa si Waafrika na shule ilibaki kuwa ya wavulana hadi mwaka 1967 ilipotaifishwa wakaandikishwa wasichana 15 lakini baadae iliendelea kuwa ya wavulana pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Shule hii ichangiwe iweze kurekebisha miundo mbinu, majengo ikiwemo kujenga upya njia ya maji taka. Mgekuwa na mipango mizuri ya kutathmini ukarabati unaotakiwa na bajeti yake. Mkakusanya michango na kuwa na utaratibu mzuri wa kuisimamia michango kupitia bodi ya shule ili ifikie ukarabati unaotarajiwa hata mimi japo sikusoma shule hiyo ningechangia. Kuhamasisha wananchi kuchangisha hela yoyote kutumia njia ya simu kunawezekane. Lakini taasisi husika ikiwemo Dawasa, jiji wasaidie kuhusu majitaka kama kuna fungu lishughulikie kutandika bomba jipya hili swala la afya za watu lishughulikiwe haraka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...