
Umati wa Washabiki wa Timu ya Simba ukiwa umefurika uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam kuipa sapoti timu yao ambayo haikuwaangusha leo,baada ya kuwatandika bao 1 - 0 watani zao wa jadi Yanga,lililotiwa kimiani kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
Beki wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan akiwania mpira na Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Simba imeshinda bao 1 - 0 lililotiwa kimiani kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Nyanda nambari moja wa timu ya Simba,Ivo Mapunda akiwa ametulia langoni kwake tayari kwa kuzuia shuti lililopigwa na Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva.
KUONA PICHA ZAIDI
mnyama oyeeee!!!!!!!!!
ReplyDelete