Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu  Kinana katika ziara hiyo ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa wa Dodoma. Kinana ataendelea  na ziara kesho katika wilaya ya Kondoa Kabla ya kuendelea katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Mbunge wa Jimbo la Chemba (kondoa kusini),na Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh Juma Nkamia akizungumza na wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Itolwa Wilayani Chemba,Mh.Nkamia kupitia Wizara yake alikabidhi hundi za fedha zenye thamani ya shilingi Milioni 52 kwa vikundi tisa vya vijana vinavyojishughulisha na  ujasiliamali.Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (pichani shoto) pia aliwahutubia wananchi hao.
 Nape Nnauye akiwahutubia Wananchi waliojitokeza  kwa wingi katika uwanja wa Itolwa wilayani Chemba mkoa wa Dodoma.
 sehemu ya umani wa Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani),wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao na kuwaasa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata nafasi ya kushiriki katika upigaji kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa.
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akiwahutubia na kuwaasa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata nafasi ya kushiriki katika upigaji kura ya maoni Katiba inayopendekezwa. 

PICHA NA MICHUZI JR-CHEMBA-DODOMA

KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi Horace Kolimba alikuwa anatokea mkoa gani? Namkumbuka sana mwanasiasa nguli huyu ....na je kuhusu kumuenzi ??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...