Mhe. Balozi Tuvako Manongi mwishoni mwa wiki alikutana na ujumbe wa wanawajeshi wanafunzi kutoka chuo cha Kijeshi (U.S. Army War Collage) ambao walikuwa katika ziara ya mafunzo. Miongoni mwa wanafunzi yupo Luteni Kanali Juma Sipe kutoka JWTZ. Ungeni huo ulitumia ziara hiyo kujifunza masuala mbalimbali yanayoihusu Tanzania kitaifa na kimataifa na uwepo wake kama nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa,
Mhe. Balozi akielezea jambo mbele ya kikundi cha wanajeshi wanafunzi ambao wapo katika mafunzo katika chuo cha U.S Army War Collage, wanafunzi hao walipata fursa ya kumuuliza Balozi maswali mbalimbali na ambayo yalijibiwa kwa ufasaha na Mhe. Balozi
Kiongozi wa Msafara akitoa zawadi yao kwa Mhe. Balozi kama kumbukumbu na shukrani yao kwa kupokelewa na kwa Balozi kutenga muda wake kukutana nao.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akiwa katika picha ya pamoja na Wanajeshi kutoka U.S Army War Collage, miongoni mwa wanafunzi hao ni Mtanzania Luteni Kanali Juma Sipe kutoka JWTZ
Mhe. Balozi Manongi akiteta jambo na Luteni Kanali Juma Sipe kutoka JWTZ ambayo yuko mafunzoni U.S Army War Collage hapa Marekani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...