Naibu
Waziri wa fedha na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba akizungumza katika
uzinduzi wa huduma ya miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB
katika hoteli ya Selena jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu mtendaji mkuu
wa Benki ya NMB Tom Borghols akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya
miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB katika hoteli ya Selena jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Sunil Colaso akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB katika hoteli ya Selena jijini Dar es Salaam leo.
Naibu waziri wa fedha na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba (katikati) akizunzindua huduma ya Airtel money na Benki ya NMB wanaoshuhudia uzinduzi huo kulia ni Kaimu mtendaji mkuu wa Benki ya NMB Tom Borghols, kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Sunil Colaso.(Picha zote na Emmanuel Massaka.
Na
Avila Kakingo Globu ya Jamii.
Wateja
wa benki ya NMB wamerahisishiwa kazi kutokana na benki hiyo kuungana na kampuni ya simu za
mikononi ya Airtel Tanzania kwenye upande
wa miamala ya fedha kwa urahisi na usalama zaidi.
Akizungumza
Naibu Waziri wa fedha na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam leo , amesisitiza kuwa huduma za Fedha kupitia
simu za mkononi ni mhimu katika kuliletea maendeleo Taifa. Mwigulu amesema kuwa ukuaji wa uchumi nchini
umewasukuma watanzania kutumia simu zao za mkononi kupata taarifa kuhusu
akaunti zao za benki popote pale walipo na wakati wowote.
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu ya Airtel,Sunil Colaso, alisema kuwa
umoja huu ni ishara ya mageuzi katika matumizi ya Teknolojia katika kuboresha
masisha ya watanzania kupitia simu za mkononi.
Kwa
njia hii wateja wa Airtel na benki ya NMB kwa pamoja wanaweza kuweka na
kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money kwenda kwenye akaunti
zao za NMB. Alisema Colaso.
Pia katika uzinduzi huo utasaidia wateja wa
Airtel kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Benki na za NMB.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...