Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania Bw. John .C. Minja wakwanza kushoto akiwaongoza Wakuu wa Magereza Wanachama ACSA (Nchi Wanachama wanaounda Taasisi zinazohusika na Urekebishaji/Magereza )Barani Afrika katika Maadhimisho ya kumaliza Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Nchini Uganda,sherehe zilizofanyika leo tarehe 9 April,2015 katika Viwanja vya Kololo Kampala Uganda.Wakwanza kulia ni Mkuu wa Magereza Nchini Angola.Maadhimisho hayo yalitanguliwa na Kikao cha siku moja cha Wakuu hao kilichofanyika jana tarehe 8 April,2015.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania mwenye nguo za kijana akisalimiana na Mgeni wa heshima katika sherehe hizo Mhe. Edward Sekandi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda,aliye mwakilisha  Rais wa  Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ndiye alipaswa kuwa Mgeni Rasmi.
 Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Nchini Uganda wakipita kwa mwendo wa haraka huku wakitoa heshima mbele ya Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe.Edward Sekandi,hayupo pichani.
  Makamu wa Rais Jamhuri ya Uganda Mhe.Edward Sekandi wa Nne kulia akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza Nchi Wanachama wa Taasisi zinazohusika na masuala ya Urekebishaji/Magereza Barani Afrika. Wanne Kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali Nchini Tanzania Bw. John C.Minja na Watatu kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Zambia Bw. Percy K. Chato.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Uganda Bw. JohnSon.O.R. Byabashaija Mafunzo hayo yameendeshwa na Chuo cha Mafunzo ya Awali ya Maafisa Magereza  Luzira.Mafunzo hayo yameendeshwa kwa muda wa miezi Tisa (9) na jumla ya Wanafunzi 1228 Wamehitimu Mafunzo na kupasishwa na Mgeni Rasmi kuwa Askari wa Magereza kwa vyeo vya Wdr kwa Wanaume na Wdrs kwa Wanawake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...