Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.
    Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank,Bw.Boyd Mwaisame akifafanua jambo  wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.
    Baadhi ya Wanafunzi wa  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu wakisikiliza kwa makini risala iliyo kuwa ikisomwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana leo Jijini Dar es Salaam.
0  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.( Picha na Emmanuel Massaka)




Na Bakari Issa,Dar es Salaam.

Benki ya Biashara ya DCB imetoa msaada wa Kompyuta kwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,kwa lengo la kutoa elimu katika Chuo hiko chenye wanafunzi wenye ulemavu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa Kompyuta kwa Chuo hicho,Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana amesema  umuhimu wa Vyuo hivi unatokana na lengo la kuanzishwa kwake aambalo ni kutoa maarifa na stadi zitakazowawezesha wananchi kujiajiri,kujitegemea  ili kuondokana na ujinga,umaskini na maradhi hatimaye waweze kuchangia kuinua uchumi wa taifa.

Pia,Dkt.Chana amewahasa wazazi kuacha kuwaacha watoto wao kukaa nyumbani bila kujishughulisha na shughuli yeyote pindi wanapomaliza masomo yao na badala yake kuwashughulisha watoto hao ili kujiepuka kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.

Kwa upande wake,Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank,Bw.Boyd Mwaisame amesema  Benki imekabidhi msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo mengi yanayojitokeza katika jamii likiwemo la ukosefu wa vitendea kazi . kwa watoto wenye Ulemavu.

Naye, Mkuu wa  Chuo hiko,Bi.Pulcheria M. Ndamgoba ametoa  shukrani kwa msaada huo wa Kompyuta katika Chuo hiko na kuahidi kukitumia vizuri katika kutoa elimu chuoni hapo,huko Kiongozi wa  Wanafunzi wa Chuo hiko,Ridhwan Omary akitoa msisitizo kwa Benki hiyo kuwasaidia kujengea viwanja vya michezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...