Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Reli
nchini(TRL),Mhandisi Kapallo Kisamfu
amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa
malipo ya Sh. Bilioni 230 ya mabehewa ya Mizigo
yenye kasoro pamoja na kufanya malipo ya
mabehewa yote kabla ya kukamilika.
Akitangaza maamuzi hayo ya kusimimishwa kwa
Mkurugenzi huyo leo jijini Dar es Salaam baada ya
ripoti ya kamati iliyoundwa na Waziri wa Uchukuzi (ambaye sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki), Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa
Uchukuzi,Samwel Sitta amesema ameshtushwa
na malipo hayo kwani yamekiuka manunuzi ya
umma kwani mkataba wake ulikuwa TRL ilipe
nusu ya asilimia 50 lakini matokeo yake
mabehewa yamelipwa yote.
Amesema mabehewa 120 yaliyofika nchini yakiwa
yana kasoro aliyazuia baada ya kubaini hivyo
lakini TRL ilikuwa imeshalipa fedha yote katika
mazingira hayo yanaonyesha mkataba una dalili
ya hujuma.
Waliosimamishwa wengine ni Mhandisi Mkuu wa
Mitambo TRL,Ngosomwile Ngosomiles,Mhasibu
Mkuu,Mbaraka Mchopa ,Mkaguzi Mkuu wa Ndani
Jasper Kisiraga pamoja na Meneja Mkuu
Ferdinand Soka.
Kamati ya uchunguzi kwa watendaji hao kwa
kuidhinishwa kwa kulipwa kwa mabilioni ya
Shilingi itaongozwa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG),Taasisi ya Kupambana
na Rushwa (Takukuru),Mamlaka ya udhibiti wa
Ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA),pamoja na
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana
kuwasimamisha baadhi ya watendaji wakuu wa kampuni ya Reli hapa nchini uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam leo.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akionyesha
baadhi ya Ripoti za uchunguzi za mamlaka ya
Bandari,TPA na Ripoti ya shirika la Reli jijini Dar
es Salaam leo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari walio hudhuria
katika mkutano wa Waziri wa Uchukuzi,Samwel
Sitta katika wizara hiyo jijini Dar es Salaam
leo.(Picha na Avila kakingo)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...