Katika jitihada za kupambana na uhalifu wa kimtandao ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kibenki katika mazingira salama zaidi, Benki ya Exim imetoa wito kwa wateja wake kuchukua kadi zao za ‘Faida chip and pin Debit Card’ zilizotambulishwa mapema mwezi Januari mwaka zilizochukua nafasi ya ‘Magnetic Stripe Faida Debit Card’.

Kadi za ‘Faida chip and pin Debit Card’ hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja ikiwa na mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki ya Exim, Bw. Eugen Masawe jijini Dar es Salaam jana, mwisho wa kuchukua kadi hizo ni tarehe 15 Aprili, hivyo wateja wamebakiwa na siku zipatazo 13 kuanzia leo.

“Tunatoa wito kwa wateja wetu kuchukua kadi zao za ‘Faida chip and pin Debit Card’ ambazo ni salama zaidi ukilinganisha na ‘Magnetic Stripe Faida Debit Card’ zilizokuwa zikitumika hapo awali.

“Wateja hawatakuwa na uwezo wa kutumia kadi zao za zamani kuanzia tarehe 15 Aprili, kwani kadi hizo zitafungiwa. Hivyo wateja wanapaswa kutembelea matawi yao ili kuchukua kadi mpya,” alisema Bw. Masawe.

Bw. Masawe alisema kuwa benki yake imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja na kusisitiza juu ya uchukuaji wa kadi hizo ambazo zitawasaidia wateja kufanya miamala yao ya kila siku katika mazingira salama zaidi.

“Kwa kutumia kadi hii mpya ya kimataifa kutoka Benki ya Exim, mteja anaweza kuwa na uhakika kwamba miamala yake inafanyika katika mazingira salama kabisa,” alisisitiza.

Aliongeza kuwa, Kadi hiyo mpya ya kimataifa inamuwezesha mteja kufanya miamala duniani kote katika mashine za ATM na POS zilizothibitishwa na MasterCard.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...