Kwa
moyo mkunjufu kabisa, nina penda kuwapongeza sana kituo cha radio
cha 93.7 EFM kwa kutimiza mwaka mmoja tangu waanze kurusha matangazo
yao hewani.
Nina
sababu nyingi za kuwapongeza lakini wakati wa kugonga “glass za cheers”
niseme hivi; Kwanza kama unatafuta mifano halisi ya ufafanuzi wa mpango wa
serikali
wa matokeo makubwa sasa (BRN) mimi nafikiri EFM ni mfano halisi.
Kwa
nini nasema hivi?
Yaami ndani
ya siku 365 tu, radio mpya imeweza kufikia nafasi ya pili kwa kusikilizwa na
nakupendwa jijini Dar es salaam kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya Geo Poll.
Lakini pia ukiangalia uongozi wa kituo hiki, ni vijana na kwa wastani umri wao
ni miaka 35, huo ni mfano mzuri kwa vijana.
Uongozi
wa EFM kwanzia Mkurugenzi Mtendaji ni Francis Ciza (Majey), Geoffrey Ndawula,
Dennis Ssebo, Dickson Ponela, Hamida Siu, Omar Ramathan na
Reuben Ndege na hao wote ni vijana tunaoishi nao mtaani lakini wamethubutu
na wameweza.
Sababu
nyingine ya kuwapongeza leo 93.7 EFM kwa kutimiza mwaka mmoja ni jinsi walivyo
buni vipindi vyao na sio ku “copy na ku paste” Nani alijua kwamba michezo
inaweza kurushwa hewani saa tatu asubuhi kila siku na kukubalika ? Sasa EFM
wana sports headquarters kila Jumatatu hadi Ijuma, huu ni ubunifu na imekuwa ni
changamoto sokoni.
Hongereni
sana 93.7 EFM,
na acha muziki uongee zaidi.
Hb day e fm,endelezeni maujanja maana sport head quarter kipindi cha michezo nina moja ya maujanja msiiachie hapo kila siku lazima mtuongozee maujanja,wapi mkude simba na dr panjuan bila kumsahau chogo chemba,I love this station.
ReplyDelete