Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
 Alhaji Dangote akiwa na viongozi wa Kijiji cha Mgao pamoja na wananchi akikagua uwanja heka mbili na nusu aliyopewa kwa ajili ya kujenga makazi yake katika kijiji hicho
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa  na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
 Msafara wa Alhaji Dangote ukielekea eneo patakapojengwa Bandari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Huu ndio unaitwa uwekezaji yaani Bilionea Dangote anaanzia chini kabisa a.k.a from scratch kujenga kiwanda pamoja na miundo mbinu kama bandari, huduma za kijamii na vitu vyote hivi vitanufaisha kampuni na jamii inayozunguka mradi huu.

    Serikali iangalie wawekezaji wa namna hii wanaoleta Matokeo Mukubwa Sasa a.k.a Big Results Now BRN wapatikane wengi zaidi mfano wenye migodi mikubwa wajenge reli kuunganisha na reli zilizopo ili kuongeza network ya reli na kutumika pia na jamii inayozunguka miradi hii mikubwa pengine kusafirisha mazao sehemu za Sumbawanga, Mchuchuma kwa kutaja kwa uchache.

    Miradi mikubwa ya wawekezaji Marekani ya Kaskazini, Ulaya, Japan na sasa ndiyo iliyofanya chachu ya network za reli zilizojengwa na wawekezaji kusafirisha makaa ya mawe, petrol, madini n.k na Tanzania inabidi kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kama Bilionea Dangote kuchangia Big Result Now.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora.

    ReplyDelete
  2. Sasa mbona mnazi uko barabarani, wekeza mwafrika tengeneza ajira kwa wenyeji, makazi hapo baada ya muda yaboreshwe na pesa ya saruji iendeleze uchumi wa Mtwara.

    ReplyDelete
  3. Hilo jina la kijiji lipo tangu asili au ni baada ya mradi kuanza?

    ReplyDelete
  4. Wafanyakazi wa kiwanda hicho na bandari kutoka Dar!

    ReplyDelete
  5. I wanna express my honest opinion on this now seemed to be a celebrated act of kindness from Mr. Dongote,I'm so concerned to allowing a foreigner to built his own private port along the shores of our country, as we know ,a port is point of entry where foreign goods or people are admitted to one country,if Mr Dongote will be allowed to built his own port and consequently not be monitored what he imports to our country ,then it will pose a dangerous threat to our security and indeed the fight against illegal drugs,how confident will we be that nothing illegal will be imported through this private harbor and how are we going to monitor what is being shipped away from this harbor? Investors are crucial to development hence economy but we shouldn't allow an investor to dictate their needs ,we have to set rules for our safety and dignity to our people otherwise people like Mr Dongote will be abusing the whole idea of free enterprise and posing a serious danger to our society

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...