Basi la Ngorika likiwa halitamaniki baada ya kugongana uso kwa uso la basi lingine la Kampuni ya RATCO katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye eneo la Kijiji cha Mbweni, Mkata mkoani Tanga. kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio,inadaiwa kwamba mpaka sasa ni Watu kumi wamepoteza maisha katika ajali hiyo, akiwepo Dereva wa Basi la Ratco.Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mpaka sasa. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga kwa maelezo zaidi.
Hivi ndivyo lionekanavyo Basi la Ratco baada ya kupata ajali hiyo leo.
Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.
Askari Polisi walifika eneo la tukio kwa Wakati ili kuhakikisha usalama unapatikana eneo hilo.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa, na inasikitisha sana.
Poleni walioathirika na ajali hii inayotisha. Basi lilivyo katika-katika ni kweli halitamaniki.
ReplyDeleteInna Lillah W.. Raajiun.
ReplyDeleteWanasheria wa tanzania mpo wapi? Mbona wananchi wanataabika kwa hizi ajali zinazozidi kila siku,kwani hakuna sheria ya kuwashitaki wenye haya makosa ?
Je insurance zinafanya nini kuhusiana na madereva wenye record mbaya?
Je idara ya vitambulisho/leseni wanaweka record hizi kwenye leseni za madereva wanaohusika na ajali?
Utakuja kusikia kisa cha ajari ni mwendo kasi au kuovateki kwenye kona
ReplyDeleteRIP
ReplyDelete