Basi la Ngorika likiwa halitamaniki baada ya kugongana uso kwa uso la basi lingine la Kampuni ya RATCO katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye eneo la Kijiji cha Mbweni, Mkata mkoani Tanga. kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio,inadaiwa kwamba mpaka sasa ni Watu kumi wamepoteza maisha katika ajali hiyo, akiwepo Dereva wa Basi la Ratco.Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mpaka sasa. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga kwa maelezo zaidi.
 Hivi ndivyo lionekanavyo Basi la Ratco baada ya kupata ajali hiyo leo.
 Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.
 Askari Polisi walifika eneo la tukio kwa Wakati ili kuhakikisha usalama unapatikana eneo hilo.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa, na inasikitisha sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Poleni walioathirika na ajali hii inayotisha. Basi lilivyo katika-katika ni kweli halitamaniki.

    ReplyDelete
  2. Inna Lillah W.. Raajiun.
    Wanasheria wa tanzania mpo wapi? Mbona wananchi wanataabika kwa hizi ajali zinazozidi kila siku,kwani hakuna sheria ya kuwashitaki wenye haya makosa ?
    Je insurance zinafanya nini kuhusiana na madereva wenye record mbaya?
    Je idara ya vitambulisho/leseni wanaweka record hizi kwenye leseni za madereva wanaohusika na ajali?

    ReplyDelete
  3. Utakuja kusikia kisa cha ajari ni mwendo kasi au kuovateki kwenye kona

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...