Na. Wambara Mayori, Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi Subira Khamis Mgalu, amewasihi wananchi wa Kisarawe kulinda ardhi yao kama mboni ya jicho na kuwataka kuacha tabia ya kuuza ardhi yao kiholela na badala yake wajikite katika kuyaendeleza maeneo yao.
Bi Subira, amesema kuwa, kuna watu hutumia kofia ya uwekezaji katika nchi hii kujitwalia ardhi katika maeneo mbalimbali na kisha kuyatelekeza bila ya kufanyiwa kazi kwa muda mrefu na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wanaoishi kuzunguka maeneo hayo kwa kugeuka kuwa mazalia na makazi ya nyoka , maficho ya wahalifu na baadaye kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi alisema.
Alisema, hatuhitaji wawekezaji wasio na tija kwa wananchi wa wilaya ya Kisarawe, na kusisitiza kuwa muda wa wawekezaji hewa umekwisha na wala hatuhitaji wawekezaji wanaokuja na mikoba bali tunawakaribisha wawekezaji wenye tija wanaoweza kutoa fursa ya ajira kwa wananchi na vijana wa wilaya ya Kisarawe.
Hata hivyo, ametoa wito kwa wenyeji na wakazi wa wilaya hiyo kutokuwa wepesi kununulika kwa watu wajanja wachache wanaojiita wawekezaji na badala yake wawe macho na watu hao ili wasijikute wanapoteza ardhi yao.
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya, amewaonya viongozi wanaokumbatia wawekezaji hewa katika wilaya hiyo na amewataka wananchi kushikamana na kushirikiana na viongozi wao wa vijiji na mitaa katika kupanga na kusimamia mipango yao ya maendeleo kwenye maeneo yao kwani maendeleo yao ni maendeleo ya wilaya ya Kisarawe, alisema.
Alisema, Bi Subira, ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Homboza kilichopo Kata ya Msimbu Tarafa ya Sungwi wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, huku akiwatahadhalisha kuwa, hakuna mtu yeyote anayeweza kumkataza ama kumnyima mtu haki yake ya kikatiba ya kuchagua kiongozi anayemtaka kwa kuwa hiyo ni haki yake na hivyo si haki kwa baadhi ya wananchi wa kijiji cha homboza, kunyimwa haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi Subira Khamis Mgalu amewataka wananchi wanaokidhi vigezo kutumia haki yao ya kikatiba kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi wakati wa uandikishaji kwenye daftari la wapiga kura na siku ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi ili kuwachagua viongozi wanao wataka bila bughudha yoyote.
kweli kabisa bi subira wape elimu hao waukae maana wanapoelekea ni pabaya bila yao wenyewe kujua, vilihi waukae mowasa?
ReplyDelete