Mwenyekiti wa bodi wa Banki ya Wananchi wa Dar es Salaam(DCB),Balozi Paul Rupia akizungumza na waandishia wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwasilisha matokeo ya uendeshaji wa benki hiyo,amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi wa Banki ya Wananchi wa Dar es Salaam(DCB),Balozi Paul Rupia akizungumza na waandishia wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwasilisha matokeo ya uendeshaji wa benki hiyo,amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Edmund Mkwawa.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi wa Banki ya Wananchi wa Dar es Salaam(DCB),Balozi Paul Rupia wakati wa kuwasilisha matokeo ya uendeshaji wa benki hiyo,amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
BENKI ya Wananchi ya Dar es Salaam (DCB) imetoa mikopo yenye dhamani ya Sh.Bilioni 363.3 kwa wajasiriamali 362,507 kati ya hao wajasiriamali wadogo kupitia vikundi ni 156,718 katika Manispaa za Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Balozi Paul Rupia amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo kwa miaka miwili, amana ilifikia sh. bilioni 113 ikiwa ni asilimia tano za amana sh.bilioni 108 ambazo zilipatikana mwaka uliopita.
Rupia amesema mikopo kwa mwaka uliopita iliongezeka kwa asilimia tisa kutoka sh.bilioni 75 hadi kufikia sh.bilioni 82.4 kwa mwaka huu na mali zimeongezeka kwa asilimia 34 kutoka sh.bilioni 117 mwaka jana na kufikia sh.bilioni 157 mwaka huu.
Amesema faida zilizopatikana kwa mwaka uliopita ilikuwa ni sh.bilioni 3.77 baada ya kutolewa kodi ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia mbili ukilinganiasha na faida ya bilioni 3.71 iliopatikana mwaka 2013.
Rupia amesema katika mikopo yote iliotolewa na benki hiyo asilimia 80 ni wanawake ambao wanajishughulisha na ujasiriamali na idadi ya wanawake imekuwa ikiongezeka kila mwaka.
Tunashukuru kwa kutoa mikopo ila tunawaomba mpunguze viwango vya riba, wengi wanashindwa kulipa madeni,na kupelekea kuwa maskini kwa kufilisiwa hata kile walichokuwa nacho babla ya mkopo.
ReplyDeleteKwa viwango vya riba vilivyopo sasa, kwa kufanya biashara halali huwezi kurudisha mkopo(unless iwe biashara haramu).
Tunaomba muangalie tena kiasi cha riba kipunguzwe,vinginevyo banks ndio zitanufaika na sio wanaokopa.