Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.

Wadau wa uwekezaji, wanasheria wa Afrika Mashariki wameunda chombo kitakachotatua migogoro mbalimbali kwa njia usuluhishi ili kuweza kukuza biashara kwa nchi wanachama.

Akizungumza leo katika Mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Chombo cha Kutatua migogoro kwa njia ya Usuluhishi (EACIA) uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki Kitengo cha Usuluhishi, Fakihi Jundu amesema kila nchi mwanachama wa Afrika Mashariki inasheria zake katika kuweza kutatua migogoro ya mikataba ya kibiashara, kunahitaji chombo cha usuluhishi nje ya mahakama katika kuhakikisha wawekezaji katika nchi mwanachama kutoathirika na uwekezaji sehemu husika.

Amesema kuwepo kwa chombo hicho ni kwa malalamiko mengi ya migogoro ya kimkataba ikiwa ni kuhusisha watalaam kila nchi katika kufanya ufumbuzi wa migogoro.

Naye Balozi wa Namibia nchini, Japhet Isaac amesema amejifunza vitu vingi jinsi na watu watakapotumia fursa hiyo katika uwekezaji katika utatuaji wa migogoro ya uwekezaji kwa nchi mwanachama wa afrika Mashariki.
Jaji Mstaafu,Thomas Mihayo akichangia maada Wadau katika Mkutano wa Kimataifa wa Kutatua migogoro ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki,Kitengo Usuluhishi,Fakihi Jundu akizungumza na vyombo vya habari katika Mkutano wa Kimataifa wa Kutatua migogoro ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Namibia Nchini,Japhet Isaac akizungumza na vyombo vya habari katika Mkutano wa Kimataifa wa Kutatua migogoro ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau katika Mkutano wa Kimataifa wa Kutatua migogoro ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...