Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale, kukabidhi barabara  ya magari yaendayo kasi kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART) ili zianze kutumika wakati sehemu zilizobaki zikiendelea kukamilika.

Hayo ameyazungumza Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli katika hafla uzinduzi wa barabara ya Uhuru ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam iliyofanyika leo katika viwanja vya Karume.

Pia Dkt. Magufuli amemwaagiza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART), Bi. Asteria Mlambo aharakishe kutafuta mabasi yaendayo kasi ili ifikapo Octoba Mwaka huu yawe yameanza kufanya kazi katika barabara ya Morogoro Road,jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.

“Tatizo la wananchi wa Dar es salaam ni kutokutunza miundombinu pamoja na kutupa taka ovyo hali inayosababisha uharibifu wa miundombinu na kupelekea mafuriko wakati wa mvua”, alisema Meck Sadick.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam jijini Dar es Salaam leo.

Sehemu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Dar es Salaam pamoja na wananchi wa Manispaa ya Ilala waliohudhuria katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Baadhi ya wananchi wa Dar ni wachafu wachafu wachafu. Kutunza mazingira ni wewe mwenyewe wala si serikali. Acheni uchafu. Dar ni kipito cha watu kutoka mataifa yote duniani. Ni aibu kwa jiji kama la Dar kushamiri kwa uchafu likishindwa na mikoa kama ya Mbeya, Njombe, Kilimanjaro, na Mwanza kwa usafi. Watu wachache wanachafua hali ya hewa ya Dar. Tujifunze usafi wa mazingira na kutotupa taka ovyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...