Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Afrika (OAU) marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho(picha na Freddy Maro).
 Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiuwasilisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo tayari kwa kuswaliwa mwili na kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
 Waumini wa Kiislam kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita tayari kwa kuswaliwa mwili na kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
 Sehemu ya waumini wa Kiislam wakisoma dua ya kumrehemu Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita aliezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...