Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Msaada kutoka Kwa Mkurugenzi wa Duka la Dawa la Nakiete Bi Batilda.
Duka la Dawa la Nakiete Limetoa msaada katika Hospitali ya Sinza.Vitu Mbalimbali vilitolewa na duka hilo vyenye Dhamani ya Shilingi milioni 6.Mkurugenzi wa Nakiete Akieleza zaidi kuhusu msaada huo amesema hiyo ni sehemu ya faida waliyopata kwa Mwaka uliopita wakaona ni vema kurudisha sehemu ya faida hiyo kwa jamii.Alisema Hospitali inakabiliwa na changaamoto nyingi lakini wao wameona wasaidie kile kidogo walichopata.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Msaada
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akiwa katikati ya wakinamama alipowatembelea kuwajulia hali na kuwapa zawadi. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akiwa wodi ya wazazi Akimpa Mmoja wa wakinamama waliojifungua jana sehemu ya zawadi zilizotolewa na Duka la Nakiete Ambapo zaidi ya wakinamama 40 waliokuwa wamelezwa katika wodi hiyo walinufaika

Baadhi ya wakina mama waliotembelewa na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Makonda
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akishukuru kwa Msaada huo amewapongeza kwa moyo waliouonyesha wa kujitolea kwajili ya wananchi maskini wa tanzania.Aidha Mkuu wa wilaya amesema Nakiete wameonyesha mfano kwa kujitolea kwasababu wa Pamoja na kulipa kodi bado wameona umuhimu wa kujitolea kwa jamii ya tanzania tofauti na wachache wanaoikosesha serikali kwa kukwepa kodi na bado hata hawawakumbuki hata Wananchi maskini wa tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...