Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango
Malecela (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja Upangaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo
ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Emma Sabaya (kushoto) leo (Jumatano,
Aprili 22, 2015) jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi
katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.
Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na TEHAMA wa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Asangye Bangu (mwenye tai ya njano)
akimweleza Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela (kulia) jinsi kumbukumbu za
waombaji wa mikopo zinavyohifadhiwa katika Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo
(Jumatano, Aprili 22, 2015). Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi
hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Hamisi
Chagonja akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.
Anne Kilango Malecela jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 22, 2015).
Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi
wa Bodi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...