Familia aliye kuwa waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine wakiwa katika ibada maalumu ya maadhimisho ya kifo chake  nyumbani kwake monduli juu, siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka
Wake wa  aliye kuwa  waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine  , wakiweka  mashada ya maua kwenye kaburi la  mume wao nyumbani kwake eneo la monduli Juu wilayani monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka.
Watoto wa kiume wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Joseph Sokoine,Tumaini Sokoine na Ibrahimu Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.

Watoto wa kike wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Seki Sokoine,Joyce Sokoine ,Mbunge wa Viti Maalum Namelock Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.
 Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akiwa na kaka yake Ibrahim Sokoine katika kumbukumbu ya kifo cha baba yao aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
 Mbunge wa Viti Maalum na Mtoto wa  aliye kuwa waziri mkuu  wa zamani   hayati Edward Moringe Sokoine, Namilock Sokoine akiongea na baadhi ya wazee wa Kimaasai baada ya misa maalumu ya maadhimisho ya kifo  cha Sokoine amabayo yalifanyika  nyumbani kwa marehemu eneo la Monduli juu wilayani Monduli mkoani Arusha jana.
 Mbunge wa viti maalu, Namelock Sokine akizungumza na wadau waliohudhuria misa hiyo Monduli Juu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duh huyu Ibrahimu ni baba yake mtupu. Namjua Joseph nilikuwa naona amefanana na baba yake ila huyu Ibrahimu ni copy na paste. RIP mzee wetu Moringe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...