Na Mwandishi Wetu

FILAMU Going Bongo ilizinduliwa rasmi juzi na kuhudhuriwa na mamia ya wadau wa filamu nchini, katika hafla iliyofanyika eneo la Bahari Zoo, jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuizindua filamu hiyo, Mwigizaji Mkuu wa Going Bongo Ernest Rwandalla alisema kuwa filamu hiyo imeshaanza kuoneshwa kimataifa zaidi kwa kuwa watu mbalimbali duniani wameanza kuifuatilia kwa njia ya I tune.

Alisema kuwa ni filamu ambayo inahusiana na suala la afya kwa hapa nchini ambapo inamuonesha mwigizaji kutoka Marekani ambae ni yeye akifanya kazi hapa nchini ya masuala ya Afya.
Alisema kuwa inaonesha ni kwa kiasi gani kuna thamani katika sekta hiyo na yeye akiwa kama mhusika mkuu ameamua kuigiza hivyo ili kuzionesha changamoto mbalimbali za sekta ya afya hapa nchini.Alisema kuwa imetumia zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuikamilisha filamu hiyo na kuwa imehusisha wasanii mbalimbali wa ndani ya nchi pia.

Alisema kuwa imehusisha maeneo kama vile Kariakoo, Sinza na kwengineko huku mahala ambapo palikuwa pakitumiwa kama hospitali ni Mwananyamala.

Kwa upande wake anaona kuwa kwa sasa kuna mafanikio makubwa katika sekta ya uigizaji hapa nchini kwa kuwa wasanii wengi wanaonesha hali ya kujituma na kufanya kazi yao kwa umakini zaidi.

" Going Bongo ni filamu ambayo inaweza kuandika historia mpya katika ulimwengu wa sanaa ya uigizaji kwa Tanzania kwa kuwa hadi sasa wapo watu wengi ambao wameanza kuiangalia filamu hii ndani na nje ya nchi" alisema.

Kwa upande wake mwigizaji mahiri wa filamu, Ahmed Olotu, Mzee Chilo ambae nae ameigiza kama mmoja kati ya wataalamu wa afya alisema kuwa filamu hiyo inaweza kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi.
" Hii ni filamu ambayo imeigizwa vema na ikiwa na kila umakini katika kuigiza na kuandikwa kwake na hata mpangilio wa habari ni mzuri pia" alisema Mzee Chiro.
 Mwigizaji Mkuu wa Filamu hiyo Ernest Rwandalla akiwa na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mantik ya filamu iko poa, lkn jina kama la kukopi vle, GOING TO AMERICA, au?

    ReplyDelete
  2. Wewe umechanganyikiwa nini Movie gani inaitwa going to America? Sasa kama zikifanana majina kuna ubaya gani na maudhui ya hiyo movie yanafanana? Au going to America na going Bongo ina sound the same kwako? Kabebe box

    ReplyDelete
  3. Naah that was Coming to America not Going. Ile alikuja Marekani kutafuta mke hii amerudi Bongo kucope na maisha na kutafuta kazi.

    ReplyDelete
  4. Acha uongo hakuja ku cope na maisha amekuja ku deliver health care akakutana na mizengwe ya Bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...