Na Mwandishi Wetu
FILAMU Going Bongo ilizinduliwa rasmi juzi na kuhudhuriwa na mamia ya wadau wa filamu nchini, katika hafla iliyofanyika eneo la Bahari Zoo, jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kuizindua filamu hiyo, Mwigizaji Mkuu
wa Going Bongo Ernest Rwandalla alisema kuwa filamu hiyo imeshaanza
kuoneshwa kimataifa zaidi kwa kuwa watu mbalimbali duniani wameanza
kuifuatilia kwa njia ya I tune.
Alisema
kuwa ni filamu ambayo inahusiana na suala la afya kwa hapa nchini
ambapo inamuonesha mwigizaji kutoka Marekani ambae ni yeye akifanya kazi
hapa nchini ya masuala ya Afya.
Alisema
kuwa inaonesha ni kwa kiasi gani kuna thamani katika sekta hiyo na yeye
akiwa kama mhusika mkuu ameamua kuigiza hivyo ili kuzionesha changamoto
mbalimbali za sekta ya afya hapa nchini.Alisema kuwa imetumia zaidi ya
mwaka mmoja na nusu kuikamilisha filamu hiyo na kuwa imehusisha wasanii
mbalimbali wa ndani ya nchi pia.
Alisema
kuwa imehusisha maeneo kama vile Kariakoo, Sinza na kwengineko huku
mahala ambapo palikuwa pakitumiwa kama hospitali ni Mwananyamala.
Kwa
upande wake anaona kuwa kwa sasa kuna mafanikio makubwa katika sekta ya
uigizaji hapa nchini kwa kuwa wasanii wengi wanaonesha hali ya kujituma
na kufanya kazi yao kwa umakini zaidi.
"
Going Bongo ni filamu ambayo inaweza kuandika historia mpya katika
ulimwengu wa sanaa ya uigizaji kwa Tanzania kwa kuwa hadi sasa wapo watu
wengi ambao wameanza kuiangalia filamu hii ndani na nje ya nchi"
alisema.
Kwa
upande wake mwigizaji mahiri wa filamu, Ahmed Olotu, Mzee Chilo ambae
nae ameigiza kama mmoja kati ya wataalamu wa afya alisema kuwa filamu
hiyo inaweza kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi.
"
Hii ni filamu ambayo imeigizwa vema na ikiwa na kila umakini katika
kuigiza na kuandikwa kwake na hata mpangilio wa habari ni mzuri pia"
alisema Mzee Chiro.
Mwigizaji Mkuu wa Filamu hiyo Ernest Rwandalla akiwa na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi.
Mantik ya filamu iko poa, lkn jina kama la kukopi vle, GOING TO AMERICA, au?
ReplyDeleteWewe umechanganyikiwa nini Movie gani inaitwa going to America? Sasa kama zikifanana majina kuna ubaya gani na maudhui ya hiyo movie yanafanana? Au going to America na going Bongo ina sound the same kwako? Kabebe box
ReplyDeleteNaah that was Coming to America not Going. Ile alikuja Marekani kutafuta mke hii amerudi Bongo kucope na maisha na kutafuta kazi.
ReplyDeleteAcha uongo hakuja ku cope na maisha amekuja ku deliver health care akakutana na mizengwe ya Bongo
ReplyDelete