Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwa ameungana na Waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front la Dar es Salaam leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika leo.

Sehemu ya Waumini wa Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu leo.
Yesu akiwa amebebeshwa Msalaba katika Igizo hilo.
Muumini wa Kikristo, Moses Kombe akitungikwa msalabani kama Yesu katika igizo lililofanywa na Vijana wa Umoja wa Kwaya zote za Usharika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Jijini Dar es salaam, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...