Na. Mwandishi Wetu

Shirika lisilo la Kiserekali la Heifer International limepokea ufadhili wa Shilingi bilioni 1.35 (USD 750,000) kutoka Starbucks Foundation ili kuwasaidia  wakulima wadogo wadogo wilayani Mbozi kupitia mradi wa Heifer unaojulikana kama “Mbozi Farmer Livelihood Improvement Project”. Fedha hizi zinatarajia kuziwezesha jumuiya za wakulima wadogo wadogo wa zao la kahawa wa nchi za Afrika Mashariki kuboresha na kuinua viwango vya maisha.

Fedha hizi ni sehemu ya mkakati wa Starbucks wa kujipatia kahawa yenye ubora madhubuti kwa kuwasaidia wakulima wa zao hilo,kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo. Mpaka sasa Starbucks Foundation imechangia  jumla ya dola za kimarekani milioni 15 ,  kwenye miradi mbali mbali ya jamii duniani.Mradi huu utakuwa ni sehemu ya Mradi wa Uendelezaji wa Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) nchini Tanzania na unatarajiwa kusaidia wakulima wadogowadogo wa kahawa wapatao 5,000.

Heifer na Starbucks walianza kutekeleza miradi pamoja zamani. Mwaka 2009 , baada ya Mkurungenzi Mkuu Howard Schultz kutembelea wakulima wadogowadogo wa kahawa nchini Rwanda; alisikiliza maombi ya wakulima – waliosema kwamba wakipata ng’ombe ; wataweza kupata Maziwa, lishe bora na kipato Zaidi kwa familia zao. Wafanyakazi wa starbucks walikusanyika kutafuta hao ng’ombe kwa ajili ya wakulima wa Rwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...