Taarifa “INAYOSOMEKA HAPA” ilitolea ufafanuzi wa Nchi ya India inavyo pambana ili kuweza kufikia malengo katika kuboresha usalama mitandao hasa katika wizi unaofanywa kupitia ATM. Na baada ya kupata kutolea ufafanuzi muswada wa sharia mtandao, taarifa “INAYOSOMEKA HAPA”  Ilifafanua yamuhimu kuzingatia ili sheria hiyo iweze kupelekea kufikiwa kwa malengo kusudiwa ya kupata Tanzania salama kimtandao na kupunguza wimbi la makosa mtandao nchini.

Baada ya hayo nilipata kuhudhuria mikutano kadhaa katika nchi mbali mbali ambapo nilifanikiwa situ kuwasilisha mada kwa wataalam wengine wa maswala ya usalama mitandao bali pia kujifunza mengi kutoka kwao katika maswala mbali mbali ya msingi ya kufanyiwa kazi ili kuweza kuboresha usalama mitandao situ katika ngazi ya kitaifa bali na kibara pamoja na  Dunia kwa ujumla.

Makubwa matatu ambayo nimeona niyazungumzie leo ni pamoja na kuhakiki kuna njia madhubuti na zenye mpango stahiki za kukuza ulewa kwa watumiaji mitandao jinsi ya kujilinda na kulinda wengine watumiapo mitandao, Kuhakikisha Taifa linakua na mikakati endelevu ya kutengeneza na kuongeza uwezo wataalam wa maswala ya usalama mitandao pamoja na kupatikana na ufumbuzi wa kudumu wa kukabiliana na wimbi la wizi wa fedha kupitia mashine za ATM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...