Ubalozi wa Tanzania, Ottawa umeshiriki kikamilifu kuandaa Mkutano wa Umoja wa Wenza wa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Canada.
Akiuwakilisha Ubalozi wetu, mwenyeji wa mkutano huo ambaye pia ni Mtunza Hazina wa Umoja huo, Mke wa Balozi wa Tanzania, Mama Esther Zoka alitumia fursa ya mkutano huo, kuvinadi vivutio vya utalii vya Tanzania, ambavyo ni pamoja na Ngororo Crater ambayo iko katika orodha ya maajabu makuu ya ulimwengu inayoratibiwa na UNESCO, Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika, visiwa vya Zanzibar, mbuga za kitalii na utalii wa utamaduni ambao umeshamiri nchini Tanzania ukiwakilishwa kikamilifu na kabila la kimasai ambalo limebahatika kuishi eneo kubwa la kitalii.
Aidha ameitangaza sehemu ya Zanzibar pamoja na kuwa ni kisiwa chenye marashi ya karafuu pia ina wanyama ambao hawapatikani mahali pengine ulimwengu. Wanyama hao ni wale Nyani Wekundu katika mbuga yetu mahili ya Jozani kisiwani Zanzibar.
Kuhusu Mlima Kilimanjaro, Mama Esther Zoka amewaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa pamoja na kwamba inafahamika kuwa watalii wanaweza kuupanda mlima huu kupitia njia mbalimbali zinazoelekea mlimani hapo, Mlima huo upo ndani ya nchi ya Tanzania katika Mkoa wa Kilmanjaro.
Amezitaja baadhi ya njia maalum zinazoweza kuwafikisha kileleni hapo kuwa ni Lemosho, Machame, Marangu, Mweka, Rongai, Shira na Umbwe.
Katika mkutano huo ambao pia ulikuwa na maonesho mbalimbali Mama balozi amelitangaza vazi la kanga la wanawake wa kitanzania kwa kugawa zawadi ya doti ya kanga kwa kila mshiriki. Aliweza kuelezea matumizi mbalimbali ya vazi la kanga ikiwa ni pamoja na kubebea watoto wachanga (receiving blanket).
Wakiwa na furaha na kujawa na hamasa, wajumbe wa mkutano huo wameahidi kupanga safari ya kuitembelea Tanzania kitalii na mwenyeji wao.
Wapili kutoka kushoto ni Mke wa Balozi wa Tanzania Ottawa Mama Esther Zoka ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa wenza wa mabalozi uliofanyika katika ukumbi wa “Tanzania House” akiwa na viongozi wenzake.
mkorogo
ReplyDelete