Kampuni ya STARMEDIA Technology maarufu kama Startimes imezindua rasmi ‘Android Application’ hii leo jijini Dar es Salaam.

Application hiyo inayofanya kazi katika simu zote zenye kutumia mifumo ya Android itakuwezesha kufahamu ratiba za chaneli zako zote kwa siku saba (wiki moja) zijazo, kuweka ‘reminders’ kwenye vipindi uvipendavyo, kuchat na watumiaji wengine wa StarTimes na kukusanya sarafu au‘coins’ zinazoweza kukombolewa na kujishindia zawadi mbalimbali.
Uzuri mwingine wa application hii iliyopewa jina la TENBRE ni kuwa haina gharama yoyote yaani ni bure kabisa. Unachotakiwa ni kuidownload kwenye simu yako kutoka Google Play, jisajili na anza kufurahia kila kinachojiri kwenye kiganja chako.

Ili kuweza kupata yote yanayojiri fuata njia zifuatazo.
1.      Hakikisha kuwa simu yako inatumia mfumo wa Android au kama simu yako ni kati ya Samsung zote, Huawei zote (isipokuwa W1 na W2), Techno zote, HTC zote, Sony, Motorola na LG.
2.      Tafuta/search Tenbre kwenye Google Play store au bofya hapa http://bit.ly/1Jv6MDn
3.      Download na install kwenye simu yako ya Android.
4.      Jaza sehemu zinazohitajika ili kujisajili.
5.      Furahia application yako.

Huu ni muendelezo wa huduma bora kutoa StarTimes kwa watanzania. Kampuni ya StarTimes Tanzania imekuwa ikitoa huduma bora na nafuu za matangazo ya digitali kwa miaka kadhaa hapa nchini. Kampuni hii inasifika kwa kuwa ndio walioleta mapinduzi ya kidigitali kwa sehemu kubwa nchini. Tunatarajia mengi mazuri zaidi kutoka StarTimes.

Kwa habari zaidi kuhusu application hii na huduma zao nyingine unaweza kutembelea moja kati ya kurasa zao mitandaoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...