Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea wikiendi hii katika viwanja sita tofauti nchini, viwanja vinne vikitimua vumbi kesho jumamosi, na michezo miwili kuchezwa siku ya jumapili.

Jumamosi JKT Ruvu watakua wenyeji wa Coastal Union katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Timu ya Mtibwa Sugar watawakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Manungu-Turiani mjini Morogoro,nayo  Ndanda FC watakua wenyeji wa timu ya Tanzania Prisons mjini Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Ligi hiyo itaendelea siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Young Africans watawakaribisha timu ya Mbeya City kutoka mkoani Mbeya, huku mjini Shinyanga katika uwanja wa Kambarage wenyeji timu ya Stand United wakiwakaribisha maafande wa  timu ya Polisi Morogoro.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...