Lori la Mizigo lenye namba za usajili T 255 CRN na lililokuwa na Tela lenye namba za usajili T 478 BCG likiwa limefunga njia baada ya kufeli breki lilipo kuwa kwenye njia kubwa katika eneo la Mbezi Mwisho, Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Dereva wa Lori hilo aliejitambulisha kwa jina moja la Bw. Sendegwa, alisema kuwa alianza safari yake ya kutoka Mkoani Singida akiwa vizuri kabisa na alipofika maendeo ya Kibamba alihisi gari yake kupoteza upepo lakini kwa wakati huo alikuwa kwenye mwendo mdogo tayari na alianza kujarubu kutafuta namna ya kusimama lakini hakufanikiwa, na alipofika maeneo ya Mbezi aliona sehemu ya kuchepuka ambayo aliona ni salama kwa upande wake na ndipo alipoamua hivyo na huko alikutana na Gari dogo aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 902 DCS ambapo alilipiga pasi ubavuni na kwenda kukita kwenye baraza la moja ya nyumba zilizokuwepo kwenye eneo hilo.Hakuna aliejeruhiwa wala kupoteza maija kwenye ajali hiyo.
Lori hilo linavyoonekana baada ya kufeli breki na kuja kusimama hapo.
Muonekano wa Prado hiyo baada ya kupigwa pasi na Lori hilo.
Ankali ipo haja ya kutundika video ya malori aina ya makubwa Land Train ya Australia ili madereva wa Tanzania wanifunze kuwa udereva bora. https://www.youtube.com/watch?v=z48bwiTf5hI
ReplyDeleteWenzenu huko Australia wanaendesha malori marefu yenye mzingo mkubwa zaidi lakini hawapati ajali za breki kufeli kila wakati. Tizama linki hii https://www.youtube.com/watch?v=yb5d6ISHoMU
Madereva mnatakiwa kuwa waangalifu kwa kusimama mara kwa mara kukagua kama matairi yemepata moto, mfumo wa breki upo ktk kiwango, trela zimejishika vizuri na mzigi(kontena) halijahama n.k
Madereva acheni visingizio.
Mdau
Diaspora
Mashariki ya mbali.
Ankali juzi juzi ulikoswakoswa barabarani, sasa wawekee video hii waone madereva wanaedesha malori marefu kupindukia na mzigo kubwa lakini wanahakikisha malori yao ni salama kila wakati yakiwa ktk mwendo.
ReplyDeleteRoad Trains on the track, Northern Territory https://www.youtube.com/watch?v=0q0TeCQ8Tec