Katika Kanisa la Living Water Centre Kawe kulifanyika mahafali ya 11 ya kozi inayoitwa Life Transforming kozi ambayo inakuwa ni darasa la kukulia maisha ya wokovu au darasa la utumishi katika Ufalme wa Mungu.

Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry Kawe  ambaye ndio kiongozi wa kozi hiyo alikuwepo kuhudhuria mahafali hayo, ambayo kozi hiyo ilianza mwaka 2004 ikiwa na wanafunzi wachache ambapo kadri miaka inavyokwenda idadi imekuwa ikiongezeka, na tangu chuo kianze mwaka huu ni mahafali ya 11.


Mahafari hayo yalipambwa na Uimbaji,Maigizo,dance na shuhuda za kile ambacho Mungu amewatendea wanafunzi hao katika kipindi chote walichosoma.Wengi wao katika shuhuda wamesema darasa hilo limewafundisha kumtumikia Mungu zaidi
Wakitoa shukrani zao kwa Mungu na mtumishi wamesema kuwa wamefundishika vyema kwa sababu wapo tofauti sana na walivyokuwa awali kabla ya kuanza darasa na wamefanyika utu upya na kwao hadi jana wanahitimu darasa wamepata mabadiliko makubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...