Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF jana ijumaa alipokea ugeni wa makamu wa Rais wa FIFA ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Jordan, HRH Prince Ali Bin Al Hussein. (picha ya Rais Jamal Malinzi na HRH Ali imeambatanishwa)
Jioni Prince Ali Bin AliHussein na ujumbe wake walifanya mazungumzo na Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi katika hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro Kempsinki) iliyopo jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo, zaidi waligusia maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya TFF na Chama cha Mpirwa wa Miguu nchini Jordan (JFA), hasa katika maeneo ya maendeleo ya mpira wa vijana, makocha na waamuzi.
HRH Prince Ali Bin Al Hussein ambaye ni mgombea wa nafasi ya urais FIFA mwaka huu, ameondoka leo mchana kurudi nyumbani kwake Jordan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...