Tamasha la Pasaka linatimiza miaka 15 toka lianzishwe hapa nchini,ambapo jumapili hii ndio linahitimishwa kwa sherehe kubwa kwenye uwanja wa Taifa kwa kushirikisa waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili kutoka, Zambia, Kenya, Rwanda, Uingereza na wenyeji Tanzania wakiwemo waimbaji nguli Solly Mahlangu na RebbecaMalope wote kutoka nchini Afrika Kusini, Mgeni rasmi katika tamasha hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikuzungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi vyakula mbalimbali kwavituo vya watoto yatima vya jijini Dar es salaam vipatavyo saba.
Baadhi ya Vyakula mbalimbali vikishushwa kwenye gari kwa ajili ya kuvikabidhi vituo vya wataoto waishio katika mazingira magumu vipatavyo saba,msaada huo una thamani ya shilingi milioni sita.
Bwa.Alex Msama akikabidhi msaada vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa Msimamizi wa kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa,Bi.Halima Ramadhan,kilichopo Boko jijini Dar.
NA LOVENESS BERNARD.
Kampuni ya Msama Promotions imetoa msaaada wa vitu mbalimbali kwa vituo 7 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Alex Msama alisema kuwa misaada hiyo ni sehemu ya mapato yatokanayo na Tamasha la Pasaka.
‘’Misaada hii ni mapato ya Tamasha la Pasaka mwaka jana ,tumewapa watoto zawadi hizi ili washiriki vema katika kusheherekea sikukuu ya Pasaka na wajisikie kama watoto wengine’’, alisema Msama.
Kwa upande wake mmoja wa walezi wa vituo hivyo Honoratha Michael ambaye ni mlezi wa kituo cha Honoratha kilichopo Temeke, alisema kuwa anaishukuru Kampuni ya Msama Promotions kwa kuwapa misaada hiyo wanaomba nawatu wengine wajitolee kuwasaidia.
‘’Tunamshukuru Msama na kampuni yake na hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuombea Baraka kutoka kwa Mungu baba pia tunawaomba watanzania wengine wajitolee kwani tunazo changamoto nyingi katika vituo vyetu’’alisema Honoratha.
Misaada hiyo iliyotolewa jijini Dar es Salaam imegharimu million sita imewanufaisha watotowa vituo vya Honoratha (Temeke),Malaika kids (Kinondoni), Umra(Magomeni),Mwandaliwa( Boko), Zaidia (Sinza)na kituo cha Rahman kilichoko Magomeni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...