11169017_958488377518759_1048095244_n
Bana ya shoo hiyo ya Gusagusa Min band na Asia Idarous Khamsin itakayofanyika nchini Uingereza

London, Uingereza
Mbunifu wa mavazi nchini ‘Mama wa Mitindo’, Asia Idarous Khamsin yupo nchini Uingereza akiwa ameambatana na magwiji wa muziki wa taarab kutoka Tanzania, Gusagusa Min Band ambao watafanya maonyesho makubwa ndani ya miji ya nchi hiyo ikiwemo London na Northampton.
Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo nchini humo, Kampuni ya Didas Entertainment ya Uingereza walieleza kuwa, shoo ya kwanza itakuwa Mei 2, katika viunga vya mji wa London na shoo nyingine ni Mei 3 katika mji wa Northampton ambapo kutakuwa na fashion shoo ‘Divas Catwalk’ itakayopambwa na Mama wa Mitindo, Asia Idarous.
11069501_10152884668557684_7139946682781219300_n
Magwji Afua, Mwanahawa, Asya Idarous na Achun Baa meneja wa Gusagusa min Band ndani ya UK.

“Gusagusa Min Band na Mama wa Mitindo, Asia Idarous, Tayari wapo ndani ya viunga vya Uingereza na wapo kamili kwa shoo kabambe Mei 2 ndani ya Empire Suite, London na shoo ya Mei 3, ndani ya Academy, mji wa Northampton. Gusagusa ipo full band nzima ikijumuisha wapiga vyombo wao” ilieleza taarifa hiyo kutoka Didas Entertainment.

Aidha, katika safari hiyo, Asia Idarous ameongozana na wadau wengine wakiwemo Mkurugenzi wa Gusagusa Mind Band, Hasan Farouk, gwiji wa taarab, Bi Afua Suleiman (muimbaji), Bi Mwanahawa Ally (muimbaji), Jaffer bhai (muimbaji), Khamis Chizi (master keyboard ) na Abdulla Ngonda (mpiga base) na wengineo wengi.
11178372_957991814235082_5347065811729573025_n
Mama wa Mitindo, Asya Idarous Khamsin (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Gusagusa Min Ban, Achun Baa na Hamis chizi 'Master keyboard' ndani ya viunga vya Milton Keynes UK (Uingereza).
Didas Entertainment imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za burudani ikiwemo kupeleka wasanii kutoka Tanzania na kupiga shoo nchini Uingereza pamoja na shughuli zingjne za Sanaa ikiwemo filamu, wasanii wa filamu na uandaaji wa filamu, ambapo hadi mwaka huu imeweza kutimiza miaka 10, tokea kuanzishwa kwake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Naomba kama ilivyokuwa awali, Taarifa za BBC Dira ya Dunia mtuwekee kwa Michuzi Blog.

    Asante sana!

    ReplyDelete
  2. Naomba kama ilivyokuwa awali, Taarifa za BBC Dira ya Dunia mtuwekee kwa Michuzi Blog.

    Asante sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...