Timu ya Wanaume Wavuta Kamba wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakivutana na Timu pinzani ya Uchukuzi (hawapo pichani) wakati wa fainali ya michezo ya Mei Mosi iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa CCM Kilumba Mkoani Mwanza leo.
 Timu ya Wanawake Wavuta Kamba wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakipambana na Timu pinzani ya Uchukuzi (hawapo pichani) wakati wa fainali ya michezo ya Mei Mosi iliyofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza leo.
 Meneja wa Timu za Michezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Suleman Kifyoga (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wavuta Kamba Wanaume wa Ofisi hiyo wakati wa Mshindano ya Michezo ya Mei Mosi yaliyofanyika Viwanja vya CCM Kilumba Mwanza
Timu ya Wavuta Kamba Wanawake kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Michezo ya Mei Mosi Viwanja vya CCM Kilumba Mwanza Aprili, 2015.
Picha na Nyamagory Omary, Afisa Habari-PMO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal,
    Mimi hukerwa sana na sisi wenye Lugha ya Kiswahili kutoandika majina na maneno kwa usahihi.

    Mfano mtu anaandika ''ata'' badala ya ''Hata''. Au anaandika jina la uwanja wa jijini Mwanza kuwa ni ''Kilumba'' badala ya ''Kirumba'' au matumizi ya herufi ''L'' badala ya ''R'' n.k.

    Tatizo hili ni kubwa sana maana hata ktk vitambulisho vya mpiga kura utaona majina ya watu wengi yameandikwa kimakosa tofauti kabisa na vyeti vyao vya shule ya msingi, sekondari, vyuo, vyeti vya kuzaliwa na hata pasipoti.

    Ankali naomba utafute nguli mmoja wa lugha ya Kiswahili awe anatusahihisha kwa makala mbalimbali ili kuweza kuandika Kiswahili fasaha na majina kwa usahihi maana naona kuna nguli wa masuala ya Kisheria ambaye pia hutusaidia sana kuelewa masuala ya kisheria kwa usahihi hapa ndani ya Globu ya Jamii.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...