Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athumani (kulia) akikabidhi baadhi ya mashuka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumo, Khatib Riwanda kwa matumizi ya Zahanati ya Kijiji hicho cha Chumo, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi. Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond.Picha na Othman Michuzi, Lindi.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athumani
akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko
wa Afya ya Jamii (CHF)
inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa
muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya
Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akieleza jambo kwa Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko
wa Afya ya Jamii (CHF)
inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo
wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo,
Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
Mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Mifuko
ya Afya ya Jamiii nchini (TNCHF), Kidani Mhenga akiwapa somo Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa wananchi hao kujua taratibu zote zinafanywa katika vituo mbalimbali vya Afya na kuhoji mapato na matumizi ya fedha za Mfuko
wa Afya ya Jamii (CHF)
inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo
wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo,
Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...