Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimuelekeza mshindi wa droo ya tatu ya mwezi wa
Aprili, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji
pia, mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam namna ya kuchomeka ufunguo wa
pikipiki katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la kampuni hiyo zilizopo
Bamaga-Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa
StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi mshindi wa simu ya kisasa aina ya Solar 5, Richard John, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya
kuibuka mshindi wa droo hiyo ya tatu ya kujishindia
pikipiki na simu ya mwezi wa Aprili inayoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati
akishuhudia ni Bw. Gideon Fumbuka ambaye naye alijinyakulia simu kisasa aina ya
P40. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia
kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia
pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis
Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama,
jijini Dar es Salaam akionyesha nyaraka
za pikipiki kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa
katika ofisi za kampuni jijini Dar es Salaam. Pamoja naye katika makabidhiano
ni Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif, kujiunga
na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia
shilingi 10,000/- na kuendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...