Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bi. Yesim Davutoglu ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili nakutoa msaada wa mashuka na nguo kwa watoto waliolazwa Hospitalini hapa. Bi. Davutoglu amesema ameguswa kutoa msaada huu kwa watoto waliolazwa na kuwatakia kupona haraka ili waendelee kukua vizuri katika jamii wanazotoka.
Watatu kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto akipokea msaada wa mashuka na nguo za watoto kutoka kwa Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bi. Yesim Davutoglu. Wa kwanza kulia ni Prof. Fatmah Alatar, Mhadhiri kutoka Uturuki ambaye kwa sasa yuko Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili (MUHAS), akifuatiwa na Dkt. Jenifa Swai Daktari Bingwa wa Watoto ambapo wa kwanza kushoto ni Muuguzi Anna Mponeja, ambaye ni Meneja wa Jengo la Watoto akifuatiwa daktari wa watoto Dkt. Helena Kakumbula.
Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bi. Yesim Davutoglu akitoa msaada kwa akina mama wenye watoto waliolazwa wodini.
Prof. Atalar na mke wa Balozi Bi. Davutoglu wakitoa msaada kwa mtoto “Musa” anayekadiliwa kuwa na umri wa miezi 18, ambaye hana wazazi. Mtoto huyu aliletwa na Polisi Hospitali ya Taifa Muhimbili miezi miwili iliyopita baada kuokotwa huko Mabibo akiwa ametelekezwa yeye na dada yake mwenye umri wa miaka mitano. Kwa sasa mtoto huyu anaendelea vizuri sana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...