Abiria zaidi ya 50 wamenusurika leo bada ya basi walilokuwa wakisafiria liitwalo Burudani kugongana uso kwa uso na Lori la tenki la mafuta maeneo ya Soni mkoani Tanga. Mashuhuda wamesema hii ajali imetokea baada ya Lori la mafuta kukatika breki na kuvaana na basi hilo uso kwa uso. Habari zinasema hakuna maafa yaliyoripotiwa hadi sasa ila watu kadhaa wamepata majeraha na kukimbizwa hospitali.
Hii ni ajali ya pili ya basi la abiria kutokea leo, ikufuatiwa na ile ya asubuhi maeneo ya Msimba, Mikumi, jirani na milima ya Udzungwa ambapo imeripotiwa kwamba watu 18 wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 10 kujeruhiwa baada ya lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na basi la abiria na yote mawili kushika moto hapo hapo.
Watu wanakufa kila siku na hawa madereva feki
ReplyDeleteDa! hadi raha kuona senema za ajali za magari mbalimbali. Na hiki ndo madereva wanavyotaka kufurahia ajali. Kwenda shule hapana ila kushuhudia ajali na vifo ndo safi kwenu. Undeni mikakati yenu wenyewe basi ili mupunguze ajali maana ile ya serikali hamuitaki. Jamani hivi watu gani wasioogopa vifo? sasa hata wapiga kura wa October wanapungua nani atachagua hao viongozi sasa. Tumrudie Mungu ni makosa yetu yanayofanya haya yote.
ReplyDelete