Wachimbaji wadogo wadogo wapatao 20 wa dhahabu katika machimbo ya madogo yaliyopo kwenye kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, wamedaiwa kufariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo hayo.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha amesema kuwa usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivamia machimbo hayo ambayo yaliachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa uimara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakaporomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao.
 Sehemu ya shimo hilo la dhahabu katika kijiji cha Kalole wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

TAARIFA KAMILI ITAWAJIA BAADAE KIDOGO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...