Mkurugenzi wa JITENG Consultant Company Bw. Andrew Huwang akiongea
jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu ushiriki wao
katika masuala ya ukusanyaji kodi na kuendelea kuongeza ushirikiano kwa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Semina iliyoandaliwa na
Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini
leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa
Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw.Yeremiah Mbaghi.
Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akiongea na jumuiya ya
wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu faida za Mfumo mpya wa
Uondoshaji Mizigo (TANCIS) unaosaidia kuongeza ufanisi katika uondoshaji wa
Mizigo ya wateja na kuondoa malamiko ya ucheleweshwaji wa huduma hiyo pia
kuondoa tatizo la upotevu na mizigo pindi inapoingizwa nchini, wakati wa Semina
iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali
za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akiwaeleza wafanyabiashara kutoka
China waishio Tanzania kuhusu umuhimu wa kushiriki katika matumizi ya Mashine
za Risiti za Kielektroniki (EFD) katika manunuzi na uuzaji wa Bidhaa mbalimbali ili
kuiwezesha serikali kupata mapato stahiki bila udanganyifu wakati wa Semina
iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali
za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam.
4-Wanajumuiya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania wakimsikiliza
Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja wakati wa Semina iliyofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Picha na HASSAN SILAYO-MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...