Ajali mbaya imetokea leo maeneo ya Makunganya, Barabara kuu ya kutoka Morogoro kwenye Dodoma baada ya gari iliyokuwa imewabeba washabiki wa Timu ya Simba Sports Club kupoteza muelekea na kuingia porini, watu nane wamepoteza maisa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya. 

Hili ni pigo kubwa sana kwa Timu ya Simba, tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Globu ya Jamii inatoa pole wa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi kuwa kuondokewa na washabiki wake hao, na Mungu aziweke Roho za Marehemu hao mahala pema Peponi, Amin.
Zoezi la uokoaji wa watu waliokuwa ndani gari hilo ikiendelea.
Muonekano wa gari hilo baada ya ajali.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani mimi ninajiuliza maswali, hivi, ni kwa nini Tanzania ajali zimezidi? je? ni barabara mbaya, magari mabovu hayafanyiwi service ya kutosha? au wanaofanya service hawana ujuzi, madereva hawana ujuzi, mimi sielewi. Kila kukicha, kila kukicha, kila kukicha ni ajali Tanzania mpaka tunaogopa sasa kusafiri. Shetani gani huyo asiye na huruma kuangamiza watu wanakosa kutimiza malengo yao kwa wakati? Tuache kumsingizia Mungu, hata siku moja Mungu hapendi watu wake waangamie, dhambi zetu ndizo zinazotufanya tuangamie, Mungu hakuumba kifo, kifo kimeletwa na kinaletwa na Mwanadamu anayekataa kutii amri za Mungu. Tumrudie Mungu na tuache viburi tuptawekwa huru kutoka dhambini. Wapumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...