Benki ya NMB imedhamini mkutano mkuu wa serikali za mitaa (ALAT) utakaoanza tarehe 8 April mpaka Tarehe 11 April, 2015 katika katika hotel ya Kunduchi beach ya jijini Dar es Salaam.

NMB imetoa shilingi milioni 150 kwaajili ya kufanikisha mkutano huo na shilingi milioni 50 kwaajili ya ununuzi wa trekta litakalotolewa kama zawadi kwa meya (Mayors Award) na halmashauri iliyofanya vizuri katika Nyanja mbalimbali kama utawala bora na utengenezaji wa miradi ya kiuchumi.

Udhamini huo unaifanya NMB kuwa wadhamini wakuu wa mkutano wa ALAT kwa mwaka wa pili mfululizo.

Hii ni mara ya pili kwa NMB kudhamini mkutano mkuu wa mwaka wa ALAT ambapo mwaka 2014, NMB ilitoa shilingi milioni 150 kabla ya leo hii kumwaga udhamini wa milioni 200 kwa mkutano mkuu wa mwaka huu wa ALAT.
Mwenyekiti wa ALAT taifa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam - Dr Didas Masaburi akitangaza maadhimisho ya mkutano mkuu wa 31 wa ALAT -2015. Pembeni ni Afisa Mkuu Fedha wa NMB – Waziri Barnabas na Katibu Mtendaji wa ALAT - Bw. Abraham Shamumoyo.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akikabidhi mfano wa hundi kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa ALAT – 2015 kwa mwenyekiti wa ALAT taifa na meya wa Jiji la Dar es Salaam Dr Didas Masaburi . Katikati ni Katibu Mtendaji wa ALAT – Bw Abraham Shamumoyo. 
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akitangaza udhamini wa NMB katika mkutano mkuu wa ALAT Taifa mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Karijee jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa ALAT taifa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam - Dr Didas Masaburi na pembeni ni Katibu Mtendaji wa ALAT - Bw Abraham Shamumoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mkutano huu utoe maazimio ya kuboresha sehemu za makazi na kumaliza kero serikali za mitaani na wakazi wanazokutana nazo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...