Familia ya Kanali mstaafu Julius L. Mugeko ya Kibaha kwa Mathias, inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki walioshirikiana nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa kijana wetu mpendwa GODFREY MWITA MUGEKO aliyefariki dunia tarehe 22 February, 2015 katika hospitali ya Tumaini Dar- es- salaam na kuzikwa tarehe 28 February, 2015 katika makaburi ya PAROKIA YA NYAMIONGO - MAKOKO MUSOMA. Familia inatoa shukrani za dhati kwa Daktari Malikita na wauguzi wa hospitali ya Tumaini, Paroko wa parokia ya Mkuza Kibaha na jumuiya ya Mt. Andrew Mtume - kigango cha Nyumbu. Paroko na jumuiya ya Mt. Yuda Thadei Parokia ya Nyamiongo Makoko Musoma, kamati za maandalizi za shughuli za mazishi Kibaha na Musoma. Tunashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu nasi kwa maombi na dua wakati wote wa kumuuguza hadi tulipompumzisha ndugu yetu. Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee, tunaomba shukrani hizi mzipokee kwa mikono miwili kutokana na jinsi mlivyohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba wa mpendwa wetu GODFREY MWITA MUGEKO. Bwana alitoa na bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. AMINA |
Home
Unlabelled
SHUKURANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...