Mwenyekiti
wa taifa wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na baraza la
uongozi wa chama hicho (hawapo pichani) iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho
jijini Dar es Salaam, wapili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif
Shariff Hamad, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Nassor Ahmed na kushoto ni
makamu Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF) Taifa,Duni Haji.
Makamu wa
kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,akisikiliza
kwa makini katika ufunguzi wa mkutano Baraza la uongozi wa chama wananchi (CUF) na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Nassor Ahmed iliyofanyika
Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
Baraza la Uongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa
CUF,Profesa Ibrahim Lipumba (hayupo
pichani) iliyofanyika leo Makao Makuu ya
Chama hicho jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo)
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya uchaguzi (NEC) ndiyo inayotakiwa kutangaza siku
ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu mwaka huu pamoja na kutangaza matokeo ya
viongozi watakao kuwa wameshinda katika uchaguzi huo.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba wakati akifungua mkutano Baraza
la uongozi wa chama hicho leo jijini Dar
es salaam. Lipumba amesema kuwa ucheleweshwaji wa uandikishaji wa daftari la wapiga kura linatia shaka kutokana na kutokukamilika kwa
zoezi hilo mpaka sasa.
Aidha amesema
kuna vifungu vya sheria kwenye katiba
pendekezwa virekebishwe hasa kifungu cha Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) kutangaza Matokeo ya uchaguzi
mkuu ya Rais atayekuwa ameshinda na awe amepata kura zaidi ya asilimia 50 pia
matokeo hayo yahojiwe au yakikishwe na
mahakama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...