Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.
Membe (Mb.) akizungumza na Mhe. Skeikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah, Naibu
Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait. Waziri
Membe alifanya ziara ya siku moja nchini humo tarehe 14 Aprili, 2015 kwa
lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Waziri Membe akimtambulisha kwa Mhe. Skeikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah, Naibu
Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait Mkurugenzi
wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya.
Mazungumzo ya ushirikiano yakiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...