Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb),akimkaribisha Wizarani Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya
Comoro, Mhe El-Anrif Said Hassane kwa mazungumzo ya kuimarisha
ushirikiano kati ya Tanzania na Comoro.
Balozi wa Comoro hapa Nchini Mhe.Dr.Ahamada El Badaoui Mohamed(kushoto)akisalimiana na Naibu Waziri Dkt.Mahadhi huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro Mhe.El-Anrif Said Hassane(katikati) akishuhudia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb),akifurahia jambo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro wakati wakiendelea na mazungumzo yao.
Katibu wa Naibu Waziri, Bw.Adam Misara (kulia) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bw.Mudrick Soragha wakinukuu mazungumzo kati ya mhe. Mahadhi na Mhe. Hassane (hawapo pichani).
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb),akifafanua jambo katika kikao hicho.
Picha na Reuben Mchome
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...