Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda,
Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier,
akipata maelezo kutoka kwa Bw. Said Ngosha Magonya, ambaye ni Kamishina wa Fedha za Nje kuhusu utaratibu
uliopangwa na Tanzania katika Mikutano hii ya majira ya kipupwe.
Mikutano ya Majira Kipupwe imeanza rasmi Mjini Washington DC.
Mikutano ya majira ya Kipupwe imeanza rasmi tarehe 14/4/2015 na
kuhudhuriwa na nchi mbalimbali wanachama zaidi ya 188.
Mikutano hii huudhuriwa
na maelfu ya wafanyakazi kutoka serikalini, waandishi wa habari, Mashirika na
Taasisi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi pamoja na kamati za kifedha.Taasisi
hizo kwa pamoja zitajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la
Fedha la Kimataifa.
Tanzania ni nchi wanachama katika
Mikutano hiyo.Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na
ni Gavana katika mikutano hii, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB),
aidha Gavana wa Benki kuu Prof. Benno
Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Imetolewa na:
Msemaji wa Wizata ya Fedha
Ingiahedi C. Mduma
14/4/2015
Washington DC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...