Wako watu wengi wameathirika
kutokana na matendo
yanayotokana na uzembe,kutojali au
makusudi ya madaktari. Wapo waliopata vilema
vya muda kutokana na
uzembe huo, wapo
waliopata vilema vya
maisha na wapo
waliouliwa na madaktari hawa hawa.
Ajabu ni
kuwa ukifanya tathmini
ya haraka utaona kuwa
watu wote waliopata madhila
kutoka kwa madaktari
huhusisha madaktari wa serikali
na katika hospitali
za serikali. Si rahisi
kukuta jambo la ajabu
la kitabibu limehusisha
hospitali binafsi. Swali
langu ni kuwa,
ewe Mtanzania daktari
amekusababishia tatizo iwe
ugonjwa wa kudumu, ulemavu
wa muda au
wa kudumu, au hata kifo
cha ndugu au
jamaa, umechukua hatua
gani baada ya tukio hilo
?. Umekaa kimya ukiwa umeridhika
au umekaa kimya
kwakuwa hujui la
kufanya ?.
1.INARUHUSIWA KUMSHITAKI
DAKTARI KWA KUSABABISHA
MADHARA KWA
MGONJWA WAKATI WA
TIBA.
Wapo wanaodhani kuwa
madaktari hawashitakiwi kwa kutomhudumia
vyema mgonjwa. Hili si
kweli daktari ni
mtumishi sawa na watumishi wengine
na kosa lolote
la uzembe, kutojali
au makusudi analofanya
na kusababisha madhara
kwa mgonjwa sheria
inaruhusu kumchukulia hatua
daktari huyo. Sawa na mtumishi
mwingine akitenda kosa kazini
anaadhibiwa ndivyo ilivyo
kwa madaktari pia. Kwa
mujibu wa sheria
daktari amepewa wajibu
wa hali ya juu
kuhakikisha anatumia taaluma
yake, weledi na
uadilifu katika kutoa
huduma ya tiba
na kuepuka kabisa
hatua au namna yoyote
inayoweza kuleta madhara
kwa mgonjwa.
Takwa hili
kwa daktari ni takwa la
kisheria na wala
si hiyari. Kwa hiyo
watu waelewe kuwa
suala la daktari
kutoa matibabu kwa
umakini ni lazima.
Kitu kikiwa lazima (mandatory) katika
sheria maana yake ni
kuwa kutofanyika kwake
hutoa haki ya
mtendewa kushitaki. Hivyo
ndivyo ilivyo kwa
madaktari. Kwa namna
yoyote anapokosa umakini
katika kutoa tiba
basi ni ruhusa
kwa mtendewa kushitaki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...